
Nina uhakika kwamba unajua Biblia ya "New International Version (NIV) ilichapishwa na Zondervan, lakini kwa sasa inamilikiwa na Harper Collins ambaye pia alichapisha Biblia ya kishetani (The satanic Bible) na kitabu kingine kijulikanacho kwa jina la" The joy of gay sex"(furaha ya mapenzi ya jinsia moja kwa wanaume).
Biblia ya (NIV) na English Standard Version (ESV) zimeondoa takribani maneno 64,575 kutoka kwenye Biblia Takatifu. Maneno hayo ni kama Jehovah, Calvary, Holy Ghost na mengine mengi. Biblia hizi (NIV, ESV) zimeondoa moja kwa moja aya ya 45. Najua unaweza usiamini lakini ndio ukweli. Naamini wengi wetu tuna Biblia mbalimbali kwenye simu, tablets, laptop au computer. Hebu jaribu kuzipitia Biblia hizo (NIV, ESV). Soma MATTHEW 17:21,18:11,23:14, MARK 7:16, 9:44, 9:46, LUKE 17:36, 23:17, JOHN 5:4, ACTS 8:37.
Hayo ni baadhi ya maandiko yaliyo ondolewa kwenye baadhi ya matoleo mapya ya Biblia. Hizo ni moja ya kampeni za shetani kuiharibu kweli ya Mungu. Ni uchakachuaji huu uliopelekea kutokea kwa dini na makanisa ya ajabu duniani, wengine wanakula nyasi, wengine wanajijeruhi miili yao hadi kutoa damu, wengine wanajisulubisha msalabani, mfano mkubwa ni kule Ufilipino . Wamesoma 1CORINTHIANS 9:27 kwenye AMPLIFIED BIBLE, "But [like a boxer], I buffet my body[handle it roughly].............".
Kumbe maneno ya Mungu yanazungumza juu ya kujitoa miili yetu kwa ajili ya kazi ya Mungu na sio kujikata kata kwa viwembe,n.k. Kazi ya shetani ni kuharibu (JOHN 10:10. Wengi wetu tanadhani kwamba matoleo hayo mapya yamerahisishwa na kueleweka vizuri, lakini zina mapungufu makubwa. Kwa sasa tunaweza kudhani kwamba hazina madhara kwa sababu zimeandikwa kwa Kiingereza, lakini jinsi siku zinavyokwenda Biblia hizo zitatafsiriwa kwa Kiswahili.
Tunza sana Biblia yako uliyo nayo baada ya kuichunguza kwamba ina maandiko yafuatayo :-
▪MATHEW 17:21
▪LUKE 17:36
▪MATHEW 18:11
▪LUKE 23:17
▪MATHEW 23:14
▪JOHN 5:4
▪MARK 7:16
▪ACTS 8:37
▪MARK 9:44
▪ACTS 15:34
▪MARK 9:46
▪ACTS 24:7
▪MARK 11:26
▪ACTS 28:29
▪MARK 15:28
▪ROMANS 16:24
Acha kutegemea Biblia za kwenye simu, laptop, tablets au computer yoyote ile maana huko ndiko wanapo chakachua Biblia kwa hali ya juu hasa wakati wa ku update Application. Kama huna Biblia fanya haraka ununue maana shetani yuko kazini kuyabatilisha maneno ya Mungu. Pia tupende kusoma sana Maneno ya Mungu ili tujue ukweli tusidanganywe bure kwa mafundisho ya uongo.
Zingatia ujumbe huu uepukane na hila hizi za mwovu anayetaka kulipoteza neno la Mungu.
No comments :
Post a Comment