Wednesday, 6 April 2016

HISTORIA YA TENZI/HYMN: "HUNIONGOZA" (HE LEADETH ME)

MWANDISHI WA WIMBO : Joseph Gilmore                       

MUZIKI UMEANDALIWA NA: William Bradbury


HISTORIA YA WIMBO/TENZI: Katika mwaka wa1862 mwezi wa 3 tarehe 26, kipindi ambacho marekani ilikuwa ikiendelea na vita ya wenyewe kwa wenyewe (civil war) nchi nzima, Mchungaji Joseph Gilmore wa kanisa la Baptist  Filadefia alisimama kuhubiri. Katika hubiri lake alitaka watu wamtazame Kristo licha ya vita iliyokuwa ikiendelea, huku akitumia maneno ya daudi mtunga zaburi katika zaburi 23 (Bwana ndiye mchungaji wangu). Baadaye
alipokuwa katika nyumba ya rafiki yake hakuacha kutafakari wazo ambalo limejengwa katika mustakabali wa Mungu kutuongoza binadamu iweje katika hali yoyote. Aliandika maneno ya wimbo "huniongoza". Miaka mitatu baadaye alipokuwa akihubiri katika kanisa lingine, alifungua kitabu na kukuta maneno yake aliyoyaandika kabla yametengenewa mziki. Bila matarajio, mke wake alituma maneno yale kwenye kituo cha kikristo cha uchapishaji ambapo William Bathelder Bradbury alitengenezea maneno yale mziki.
FUNGU BIBLIA:   Zaburi 23:1-3Bwana ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu. Katika malisho ya majani mabichi hunilaza, Kando ya maji ya utulivu huniongoza. Hunihuisha nafsi yangu; na kuniongoza Katika njia za haki kwa ajili ya jina lake.






TENZI ZA ZIADA
IMEANZISHWA HUKUMU 
MWANDISHI WA WIMBO/HYMN:  Franklin E. Belden



NINAO WIMBO MZURI
 MWANDISHI WA WIMBO/HYMN: Edwin Othello Excell (1851-1921)




No comments :

Post a Comment