Saturday, 9 April 2016

HUKUMU



Je umekuwa ukijiuliza juu ya hukumu? Fuatilita somo hili.
 Fungu: (Ufunuo 20:12). "Nikawaona wafu wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi na vitabu vikafunguliwa na kitabu kingine kikafunguliwa ambacho ni cha enzi na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu sawa sawa na matendo yao."
            Kumekuwa na dhana mbali mbali juu ya hukumu. Wengine wamedai kuwa hakuna hukumu, wengine wakidai Mungu ana upendo sana (jambo amblo ni kweli) na hivyo hawezi kuhukumu binadamu kifo hata ikiwa wametenda dhambi. Wengine wamekuwa wakidhihaki huku wakidai hakuna kitu kama hukumu kwani imemchukua Kristo miaka mingi na hadi leo hajarudi. Usichukuliwe na dhana hizi mpendwa biblia ipo wazi na hata sasa hukumu inae
ndelea. (1 Petro 4:17) “Kwa maana wakati umefika wa hukumu kuanza katika nyumba ya Mungu; na ikianza kwetu sisi, mwisho wao wasioitii injili ya Mungu utakuwaje?”
Hukumu ni kwa waliotenda mema au mabaya?
(2 wakorintho 5:10) “Kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mtu apokee ijara ya mambo aliyotenda kwa mwili, kadiri alivyotenda, kwamba ni mema au mabaya.” Hivyo hukumu ni kwa wote watenda mema na mabaya. Danieli naye anaongezea katika (Danieli 12:2) “  Tena, wengi wa hao walalao katika mavumbi ya nchi wataamka, wengine wapate uzima wa milele, wengine aibu na kudharauliwa milele.” Hivyo wemgime watahukumiwa uzima wa milele huku wengine wakihukumiwa kifo yaani aibu ya milele.
Danieli na vitabu vikifunuliwa kwa ajili ya hukumu hiyo, (Danieli 7:9-10).  “Nikatazama hata viti vya enzi vikawekwa, na mmoja aliye mzee wa siku ameketi; mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji, na nywele za kichwa chake kama sufu safi; kiti chake cha enzi kilikuwa miali ya moto, na gurudumu zake moto uwakao. Mto kama wa moto ukatoka ukapita mbele zake; maelfu elfu wakamtumikia, na elfu kumi mara elfu kumi wakasimama mbele zake; hukumu ikawekwa, na vitabu vikafunuliwa. 
Ni watu wa umri gani watahukumiwa?
(Ufunuo 20:12) “Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao.” Watu wa rika zote watahukumiwa.
Je hukumu itahusisha mambo gani?
(Mathayo 12: 36)  “Basi, nawaambia, Kila neno lisilo maana, watakalolinena wanadamu, watatoa hesabu ya neno hilo siku ya hukumu”.
Siri zetu zote zitaletwa hukumuni, (Warumi 2:16)   “katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu, sawasawa na injili yangu, kwa Kristo Yesu.”
(Muhubiri 12:13) “Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, Maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu. Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya.”
Je inakuhitaji kuwa na dhambi kiasi gani ili uhukumiwe kifo cha milele au uzima wa milele?
Dhambi moja tu hata iwe ndogo kiasi gani inaweza kukusababishia usiingie kwenye ufalme wa Mungu. (Yakobo 2:20,11) “Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote. Kwa maana yeye aliyesema, Usizini, pia alisema, Usiue. Basi ijapokuwa hukuzini, lakini umeua, umekuwa mvunja sheria.” (Mathayo 12:36).  Basi, nawaambia, Kila neno lisilo maana, watakalolinena wanadamu, watatoa hesabu ya neno hilo siku ya hukumu.
Je tunawezaje kuepuka hukumu ya kuangamizwa na kupotea juu ya uso wa nchi milele?
Walinaomtumainia Kristo, kumwamini na kushika maagizo yake na amri zake ndio watakaokolewa. (Danieli 12:1) “Wakati huo Mikaeli atasimama, jemadari mkuu, asimamaye upande wa wana wa watu wako; na kutakuwa na wakati wa taabu, mfano wake haukuwapo tangu lilipoanza kuwapo taifa hata wakati uo huo; na wakati huo watu wako wataokolewa; kila mmoja atakayeonekana ameandikwa katika kitabu kile.”  
Ingalipo nafasi hatuna haja ya kuendelea lidumu katika dhambi. Hata kama tumefanya dha,bi kiasi gani, ingalipo nafasi ya kutubu, Kristo anasubiri leo ufanye maamuzi ya kuiacha dhambi ukajiunge na kundi la watakatifu watakaoishi milele na milele baada ya zama zile za hukumu. Mpatanishi tunaye ambaye ni Yesu Kristo. (1Timotheo 2:5) “ Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu.”  (1 Yohana 1:9) “ Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.” Mungu aliahidi jambo kwa Isaya kuhusu wadhambi; (Isaya 1:18) “Haya, njoni, tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.” (Isaya 45:25) “Mimi, naam, mimi, ndimi niyafutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe, wala sitazikumbuka dhambi zako.”
Ni lini Kristo atakuja kuhukumu ulimwengu?
Siku Kristo anapokuja haijuliani na ndio maana inatubidi muda wowote tuwe tayari, hakunaanayejua maisha yake yatakoma lini (maana baada ya kufa hakuna njia nyingne yoyote ya mwanadamu kuokolewa), wala hakuna ajuaye Kristo anakuja lini. Hivyo basi yatupasa kujiweka tayari kila muda na kila wakati. (Mathayo 24:36) “Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake.”
Hivyo jiweke tayari kumlaki Kristo ajapo mawinguni. Kwa nini usichague leo kumpokea Kristo na kuishi kama apendavyo ili uepuke hukumu ya kifo cha aibu milele. Njoo leo naye Kristo atakupokea
MUNGU AKUBARIKI UNAVYOTAFAKARI NENO LAKE



No comments :

Post a Comment