Saturday, 9 April 2016

HUKUMU



Je umekuwa ukijiuliza juu ya hukumu? Fuatilita somo hili.
 Fungu: (Ufunuo 20:12). "Nikawaona wafu wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi na vitabu vikafunguliwa na kitabu kingine kikafunguliwa ambacho ni cha enzi na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu sawa sawa na matendo yao."
            Kumekuwa na dhana mbali mbali juu ya hukumu. Wengine wamedai kuwa hakuna hukumu, wengine wakidai Mungu ana upendo sana (jambo amblo ni kweli) na hivyo hawezi kuhukumu binadamu kifo hata ikiwa wametenda dhambi. Wengine wamekuwa wakidhihaki huku wakidai hakuna kitu kama hukumu kwani imemchukua Kristo miaka mingi na hadi leo hajarudi. Usichukuliwe na dhana hizi mpendwa biblia ipo wazi na hata sasa hukumu inae

Wednesday, 6 April 2016

HISTORIA YA TENZI/HYMN: "HUNIONGOZA" (HE LEADETH ME)

MWANDISHI WA WIMBO : Joseph Gilmore                       

MUZIKI UMEANDALIWA NA: William Bradbury


HISTORIA YA WIMBO/TENZI: Katika mwaka wa1862 mwezi wa 3 tarehe 26, kipindi ambacho marekani ilikuwa ikiendelea na vita ya wenyewe kwa wenyewe (civil war) nchi nzima, Mchungaji Joseph Gilmore wa kanisa la Baptist  Filadefia alisimama kuhubiri. Katika hubiri lake alitaka watu wamtazame Kristo licha ya vita iliyokuwa ikiendelea, huku akitumia maneno ya daudi mtunga zaburi katika zaburi 23 (Bwana ndiye mchungaji wangu). Baadaye

Tuesday, 5 April 2016

JE SIKU YA SABATO NI IPI?

Jibu hili hapa:
Yesu alifufuka siku ya kwanza ya juma ambayo ni jumapili kama umma wote wa wakristo unavyoamini, Luka. 24:1-3, “Hata siku ya kwanza ya juma, ilipoanza kupambazuka, walikwenda kaburini, wakiyaleta manukato waliyoweka tayari. Wakalikuta lile jiwe limevingirishwa mbali na kaburi, Wakaingia, wasiuone mwili wa Bwana Yesu"                                      
Na hivyo siku ya kwanza ya juma ni jumapili na hivyo siku ya saba inaangukia jumamosi ambayo sabato ya Bwana.

PLEASE FORGIVE ME- GOLDEN ANGELS


SIRI YAFICHUKA: NI KUHUSU KUTOKUWEPO KWA BAADHI YA MANENO NA MAFUNGU KATIKA BIBLIA YA NEW INTERNATIONAL VERSION (NIV) NA ENGLISH STANDARD VERSION (ESV)


https://redeeminggod.com/wp-content/uploads/2011/04/burning_bible.jpg 

Nina uhakika kwamba unajua Biblia ya "New International Version (NIV)  ilichapishwa na Zondervan, lakini kwa sasa inamilikiwa na Harper Collins ambaye pia alichapisha Biblia ya kishetani (The satanic Bible) na kitabu kingine kijulikanacho kwa jina la" The joy of gay sex"(furaha ya mapenzi ya jinsia moja kwa wanaume).
Biblia ya (NIV) na English Standard Version (ESV) zimeondoa takribani maneno 64,575 kutoka kwenye Biblia Takatifu. Maneno hayo ni kama  Jehovah, Calvary, Holy Ghost na mengine mengi. Biblia hizi (NIV, ESV) zimeondoa moja kwa moja aya ya 45. Najua unaweza usiamini lakini ndio ukweli. Naamini wengi wetu tuna Biblia mbalimbali kwenye simu, tablets, laptop au computer. Hebu jaribu kuzipitia Biblia hizo (NIV, ESV). Soma MATTHEW 17:21,18:11,23:14, MARK 7:16, 9:44, 9:46,  LUKE 17:36, 23:17, JOHN 5:4, ACTS 8:37.

SOMO: KIFO

Je unajua? Je umewahi kujiuliza?
Mtu akifa anaenda wapi? Je anaenda mbinguni? je anaenda motoni? Je anaenda Purgatory?

Biblia kamwe haikutuficha. Mungu aliweka bayana mwanzo kabisa baada ya kuumba dunia. "lakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya, usile, maana siku utakapokula matunda ya mti huo, hakika utakufa.” (Mwanzo 2:17).

Lakini shetani aliingilia na kuwadanganya Adamu na Hawa. "lakini Mungu alisema, ‘Msile matunda ya mti ulio katikati ya bustani, wala msiuguse, msije mkafa. Nyoka akamwambia mwanamke, “Hamtakufa!" (Mwanzo 3:3,4). Na hili ndilo fundisho la umizimu linaloendelea hadi sasa ya kwamba mtu akifa anaenda kuishi mbinguni kama akitenda mema na anaenda kuchomwa moto akiwa kuzimu (zingatia muda anachomwa moto yupo hai) au Purgatory anapotakaswa dhambi., haya ni baadhi ya mafundisho ya umizimu na uongo ambayo alianzisha shetani edeni!